Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amemjia juu msanii mwenzake Diamond Platnumz na kumtaka aache vitendo vyake anavyofanya vinavyopelekea kudhalilisha wanawake.
Nuh ameongelea kitendo cha Diamond kusabaza video Kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wanawake wawili tofauti katika usiku mmoja kama udhalilishaji wa wanawake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Nuh Mziwanda amedai kitendo alichokifanya Diamond sio cha kiungwana kwani wanawake wote ni kama mama zetu hivyo tunapaswa kuwaheshimu.
"Ni lazima tuwaheshimu wanawake maana ndio waliotuzaa na waliotuleta duniani kwahiyo automatically ni watu wa kuwaheshimu na hiyo ni nguvu ambayo Mwenyezi Mungu kaiweka ......kwaiyo huwezi ukarekodi vitu kama vile alafu ukaviweka Kwenye mitandao inakuwa inaleta picha mbaya kama vile dada zetu hawana thamani kitu ambacho sio cha kweli”.
Tangu kitendo hiko kitokee siku chache zilizopita tayari Diamond ameshachukuliwa hatua za kisheria na Waziri Mwakyembe amehaidi atafikishwa mahakamani
Post A Comment: