Klabu ya Singida United imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup – ASFC), baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye dimba la Namfua mjini Singida.
Waliyokuwa mwiba mkali katika mchezo huo ni Hassan Matelema aliyeanza kuipatia bao la kuongoza timu yake ya JKT Tanzania dakika ya 38 kisha Singida United ikasawazisha goli hilo dakika ya 54 kupitia kwa mchezaji wake, Tafadzwa Kutinyu kisha huyo huyo kuhitimisha karamu hiyo ya magoli dakika ya 98 na kumalizika kwa matokeo hayo ya 2 -1.
Singida United sasa itakutana na Mtibwa Sugar hatua ya fainali mchezo utakao pigwa kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha Juni 2, 2018.A
Post A Comment: