Mwenyekiti
wa Bodi ya Tanzania Microfinance Association (TAMFI), Joel Mwakitalu
(kulia) akikabidhi cheti kwa mshindi wa tatu wa tuzo za Ujasiriamali za
Citi Foundation, Lydia Majoro wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini
Dar es Salaam.
Mjasiriamali
mlemavu aliyefanya vyema Aneth Geraw ambaye aliondoka na kitita cha
dola za Marekani 2000 wakati hafla ya kukabidhi tuzo za ujasiriamali za
Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) akikabidhi cheti kwa
mshindi wa pili wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Anney
Sekulasa (kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Anayeshuhudia tukio hilo katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) na Mkurungenzi wa Fedha
na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (katikati)
kwa pamoja wakikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Yetu
Microfinance, Attemius Millinga (kushoto) ambapo taasisi yake imekuwa na
ubunifu mkubwa wa bidhaa zake sambamba na mifumo ya kutolea huduma na
methodolojia wakati wa hafla fupi ya tuzo za ujasiriamali za Citi
Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanamke
aliyefanya vyema kwenye ujasiriamali mdogo, Lucy Kiongosi akipozi baada
ya kupokea cheti kilichoambatana na dola za Marekani 2000 wakati wa
hafla ya tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika mwishoni
wa wiki jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila na kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso.
Mshindi wa tatu wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Lydia Majoro akifurahi na kupozi na cheti pamoja na tuzo yake.
Mkurungenzi
wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila
(katikati) akikabidhi cheti kwa Mjasiriamali mdogo aliyefanya vyema
mwenye umri wa miaka 18-25 tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation,
Mopaya Madi (kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es
Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank,
Joseph Carasso (kulia).
Mshindi
wa jumla wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation Afisa Mtendaji Mkuu
wa kampuni ya Beula Seed and Co & Sons, Zabron Mbwaga (kushoto)
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania
Microfinance Association (TAMFI), Joel Mwakitalu (wa pili kushoto),
Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander
Mwinamila (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph
Carasso (kulia).
Mkurugenzi
Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) akikabidhi cheti kwa
Ofisa mikopo Rose Chacha (kushoto) wakati wa hafla fupi za tuzo za
ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Anayeshuhudia tukio hilo ni ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki
Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila.
Na Mwandishi Wetu
Zabron
Mbwaga ambaye ni Mzalishaji mbegu, aliyepo Viwanja vya NaneNane, Njiro
mkoani Arusha ametwaa tuzo ya mshindi wa jumla wa tuzo za Ujasiriamali
ya Citi Foundation. Tuzo hiyo inaambatana na fedha taslimu dola za
Marekani 7,500.
Mbwaga
ambaye aliwezeshwa upanuzi wa shughuli zake kwa mikopo kutoka BRAC
Tanzania, alianza kazi zake akiwa na mtaji wa shilingi milioni 2 kabla
ya kuongezewa nguvu na BRAC. Tuzo hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki zilitolewa kwa wajasiriamali 16 na ofisa mikopo mmoja.
Mshindi
wa pili ni Anney Sekulasa akiondoka na dola za Marekani 6000 huku
mshindi wa tatu ni Lydia Majoro ambaye aliondoka na dola za Marekani
4000. Nafasi ya mjasiriamali mlemavu ilitwaliwa na Aneth Geraw aliyepata
dola za Marekani 2000.
Zaidi
ya shilingi milioni 70 za kitanzania zimetolewa kwa washindi wa kwanza
hadi wa 16 . Pia Taasisi za kifedha za wajasiriamali wadogo na wa kati
(MFI) zenye ubunifu mkubwa wa bidhaa zake na huduma, mifumo ya kutolea
huduma na methodolojia pia ilipata tuzo. Safari hii Yetu Microfinance
ndio walioinyakua.
Tuzo
hizo za Citi Bank Foundation zimeendeshwa na Mtandao wa Asasi zinazotoa
huduma za kifedha kwa wajasiriamali wadogo (TAMFI) ‘TAMFI’ na washindi
wametangazwa na majaji walioshiriki kufanyakazi hiyo.
Tuzo hizo zimelenga kuhamasisha wajasiriamali kutumia taasisi za kifedha za watu wa kati na chini na kufaidika nazo. Takribani
wajasiriamali 209 waliwasilisha miradi yao lakini 22 pekee ndio
waliweza kupenya na 16 ndio walipata ushindi wa tuzo tofauti.
Safari
hii washiriki walitoka maeneo mbalimbali nje ya Dar es Salaam tofauti
na ilivyokuwa kwa mwaka 2016 ambapo washiriki wake walikuwa ni wa Dar es
Salaam pekee.
Washindi
wengine ni Comelord Swai $ 1000, Prisca Kayombo $ 1000, Rahim Kalyango
$ 1000, Emmanuel Lazaro $ 1000, Jumanne Findisha $ 1000, Salma Said $
1000, Editha Lukindo $ 1000, Amon Kalumuna $ 1000, Salum Chumu $ 1000 na
Doroth Sambi $ 1000.
Post A Comment: