Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Tumaini Jipya - New Hope na Diwani wa Kaunti ya Leicestershire Jimbo la Blaby nchini Uingereza, Louise Richardson amekutana na Katibu Tawala mkoa wa Arusha, kwa ajili ya kujadili maendeleo ya mradi wa maji wa vijiji vitano, unaotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Arusha.
Diwani Louse ambaye ndiye chimbuko la mradi huo, baada ya kuishi katika kijiji cha Lengijave kata ya Olkokola kama Volunteer na kshuhudia adha kubwa ya maji inayowakabili wananchi wa Olkokola.
Akizungumza na mgeni huyo Ofisini kwake, Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Richard Kwitega amesema kuwa, kwa sasa mradi huo uko katika hatua za uchimbaji wa visima, usanifu na upembuzi yakinifu na unategemea kukamilika mwezi Septemba, 2018.
Aidha Kwitega amemshukuru Diwani Louise, kwa kuiunga mkono serikali ya Tanzania kwa kuwahudumia wananchi na kuahidi kutoa ushirikiano kwa Shirika la Tumaini Jipya -New Hope wakati wote linapofanya kazi zake katika mkoa wa Arusha.
Hata hivyo Mhaidiolojia katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Ngubila Kilyamalago amepata fursa ya kumuonesha mgeni huyo, usanifu wa mradi mzima pamoja na michoro ya mradi huo kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja wa mradi huo.
Louise ameridhishwa na hatua zilizofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi huo na kusema kuwa mpaka sasa amepata mwanga wa wananchi kupata huduma za maji na kufikia lengo lake alilolikusudia.
Mradi huo wa vijiji vitano maarufu kama mradi wa WaterAid unatekelezwa kwenye kijiji cha Olkokola, Lengijave na vitongoji vya Seuri, Ekenywa na Ngaramtoni vya Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni, kwa unafadhiliwa na Idara ya Maendeleo ya Uingereza DFID kwa gharama ya shilingi Bilioni 4.5
Post A Comment: