Usiku wa kuamkia Aprili 9, watoto wawili wa familia moja, Mussa Baraka (2) na Mariam Simoni (4) walifariki dunia kwa  kuangukiwa na ukuta wa nyumba walimokuwa wamelala katika Mtaa wa Buguku eneo la Buhongwa jijini Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema watu watatu akiwamo mama mzazi wa watoto hao, Dabacha Simon; bibi yao, Linda Kulwa na kaka yao, Simon Samson (5) walijeruhiwa katika tukio hilo lililotokea saa nane usiku na kulazwa katika hospitali ya Wilaya ya Nyamagana ya Butimba.
Pia, Usiku wa kuamkia leo April 17, mtu mmoja amefariki dunia baada ya nyumba yake kubomoka na kuanguka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Tukio hilo limetokea Kata ya Kiseke mtaa wa Kabambo Wilaya ya Ilemela. Aliyefariki ametambulika kwa jina moja la  Laurent 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: