Hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho 'Azam Sports Federation CUP' inaanza kutimua vumbi leo kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.

Stand United watakuwa wenyeji watakapokuwa wanaikaribisha Mtibwa Sugar kutoka mjini Morogoro ambao wametamba kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amesema wao wana uzoefu kuliko Stand hivyo wanaamini wataweza kuiondosha Stand na kuweza kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa.

Kumekuwa na majigambo pia upande wa Stand United ambao wanatamba kupata matokeo kuelekea hatua ya fainali ya michuano hiyo.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni ambapo yatakuwa yanarushwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: