Mshambuliaji wa Taifa Stars na klabu ya Difaa El Jadid, Simon Msuva ameendelea kung’ara kwenye ligi kuu ya Morocco.
Mshambuliaji huyo jana (Jumapili) amefanikiwa kuifungia timu yake hiyo bao moja kati ya ushindi wa mabao 2-1 walioupata katika ligi kuu dhidi ya Raja Casablanca.
Msuva alifanikiwa kufunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 76 ya mchezo huo huku goli la kwanza likifungwa na Ahaddad H dakika ya 45. Wakati huo huo bao la Raja Casablanca lilifungwa wa njia ya penalti na Iajour M dakika ya 41 ya mchezo huo.
Mchezo huo uliocheza kwenye uwanja wa Stade Ben Ahmed El Abdi (El Jadida (Mazghan)).
Post A Comment: