Wasanii
maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Ali Kiba
wamekutana katika msiba wa Agnes Masogange na kusalimiana.
Mara
baada ya wasanii hao kusalimiana kwa kupeana mikono wakiwa katika meza
kuu, waombolezaji waliojaa kwenye Viwanja vya Leaders walipiga kelele.
Diamond
alimsalimia Kiba kwa kumpa mkono, kisha wawili hao walikumbatiana na
baada ya tukio hilo, MC Pilipili alisikika akisema: “Unaona sasa, hawana
ugomvi hawa.”
Kumekuwa
na taarifa za wanamuziki hao kuwa na ugomvi kwa muda mrefu ambao hata
hivyo, unatajwa kutengenezwa na mashabiki wao wa ‘Team Kiba na Team
Diamond.’
Akizungumzia
katika viwanja hivyo, Ali Kiba ambaye ametoka kuchukua jiko hivi
karibuni, amesema harusi na kifo vyote ni ibada na ndiyo maana amefika
kuungana na waombolezaji wengine ingawa bado yupo fungate.
Masogange alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge ambako alilazwa kwa siku nne.
Post A Comment: