Hapo jana April 22, 2018 mwili wa marehemu Agness Gerald ‘Masogange’ aliagwa katika viwanja vya Leaders Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya maziko.

Katika tukio ya kuaga yalitokea matukio mbali mbali ambayo yaliibua mijadala ya hapa na pale. Kitendo cha Diamond na Alikiba kupeana mikono liliweza kugonga vichwa vya habari kwa kiasi chake.
Tukio ambalo linagonga vichwa vya habari kwa sasa hasa mtandaoni ni lile la msanii wa Bongo Movie, Rammy Gails kuzimia lakini mkononi bado kashikilia kwa nguvu kitambaa chake. Watu wanahoji inawekana vipi?, sisi hatujui.
Msanii wa Bongo Movie, Irene Paul, Mchambuzi wa soka, Edo Kumwembe na msanii wa hip hop, Wakazi ni miongoni mwa wale walianzisha mijadala katika mitandao kuhusiana na ishu ya Rammy Gails.
Irene Paul Maskini pamoja na kuzimia/kuishiwa nguvu lakini aliweza kuwa na nguvu ya kushika vitu vyake… wote tumeguswa lakini pia tusifanye msiba ya wenzetu kama sehemu ya kupata kiki zetu!! TUIHESHIMU kama kweli tuna malengo mema ya kumsindikiza mwenzetu kwa upendo, na zaidi tujue kutofaufisha kati ya LOCATION ZA FILAMU na DUNIA YA UKWELI.
Kuna vitu havikeri ila VINACHEFUA!! I am sorry to say umenichefua leo.. na bora ungekuwa Jinsia yetu angalau!! Ningelala na hili ningekabwa!! Pumzika kwa Amani AGNES!!(BONGO MOVIE WENGI UZURI TUNAJUANA NA HAPA TUMEELEWANA).
Edo Kumwembe Katika ubora wao..Bongo Movie..katika msiba wa Masogange .mtu kazimia huku akiendelea kushikilia kitambaa chake mkononi…nawakubali sana hawa jamaa…wanaweza kuigiza wapo Dar lakini wanapanda Mlima Kilimanjaro…
Wakazi Ladies and Gentlemen, welcome to BONGO MOVIE…. unazimia ila bado mkono umeshikilia mali zako. This defies all laws, hypothesis and theories of science.
Kwa sinema kama hizi ukisikia Mtu kauliwa ili mwingine akiki, inakuwa rahisi sana kuamini.
Video vixen Agness Gerald ‘Masogange’ alifariki April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam, enzi za uhai wake aliweza kutokea kwenye video za wasanii kama AY na Mwana FA, Belle 9, Tunda Man, Izzo Bizness, Barnaba na wengineo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: