Hakuna ubishi kwamba Cassper Nyovest ni miongoni mwa marapa wakubwa zaidi Afrika Kusini kwa sasa kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye muziki toka mwaka 2009, alipoanza kujulikana zaidi.
Kwa Afrika Kusini, ndiye mwanamuziki pekee aliyefanikiwa kujaza mashabiki kwa shoo ya peke yake kwenye uwanja wa michezo wa Dome unaobeba watu 20,000 (mwaka 2015) na mwaka 2016, wanja wa Orlando, wenye uwezo wa kubeba watu 40, 000.
Msanii wa miondoko ya Hip Hop kutoka South Africa, Cassper Nyovest |
Lakini pia kwa ngoma kali zikiwemo Doc Shebeleza, Tsibip, Mpumakim na Mama I Made pamoja na kolabo kubwa zikiwemo alizofanya na wanamuziki Vee Money (Tanzania), Diamond Platnumz (Tanzania), Davido (Nigeria), Talib Kweli (Marekani), The Game (Marekani) na Casey Veggies (Marekani), tunaweza kuelewa ni kwa nini jamaa ameweza kuliteka gemu la Muziki wa Hip Hop, Afrika.
Nyumba
Kwa Cassper, mkwanja mrefu anapata kupitia shoo, mauzo ya albamu, kampuni yake ya Familly Tree, ambayo ni lebo ya muziki pamoja na media ya habari, dili kutoka kwa makampuni ya Castle Lite, KFC, MTN, AG Mobile pamoja na kinywaji cha Ciroc Vodka, ambacho anakitangaza.Utajiri wake kwa jumla unatajwa kufikia dola za Kimar-ekani milioni 3 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 6.8 za Kitan-ania.
Wengi wana-weza kujiuliza kutokana na fedha zake maisha yake ya ‘luxury’ yanakuwaje, vipi kuhusu nyumba, magari anayoendesha na vitu vingine, sasa sikia;
Mbali na kumiliki majumba kadhaa ikiwemo aliyowanunulia wazazi wake, Cassper, nchini Afrika Kusini anaishi huko Kyalami, jijini Johannesburg, kwenye jumba lenye vyumba vingi, studio pamoja na bwawa la kuogelea lililomgharimu takribani Randi milioni 10 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.8.
Magari
Rapa huyu anayemiliki albamu kadhaa zikiwemo Refiloe, Tsholofelo na Doc Shebeleza, anamiliki magari kadhaa yakiwemo BMW, magari mawili aina ya Bentleys na Rolls Royce.
Ndege binafsi
Cassper anaendelea kuonesha kwamba ni mtu anayependa vitu vizuri. Sasa kwa Afrika ni rapa pekee anayemiliki ndege binafsi aina ya King Air B200 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 1.7, (zaidi ya bilioni 3) aliyonunuliwa na kampuni ya kinywaji cha Ciroc Vodka mara baada ya kuingia nao mkataba.
Pamoja na yote hayo kutokana na kukua kwa muziki wake, akiwa na miaka 27 tu, Cassper anatazamiwa kuwa miongoni wa wanamuziki matajiri zaidi Afrika ndani ya miaka michache ijayo kutokana na kipato chake kukua kwa kasi.
Katika miaka miwili iliyopita, utajiri wa Cassper ulikuwa unatajwa kuwa dola za Kimarekani 800,000 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1. 8, lakini kwa sasa yupo mbali zaidi kutokana na dili anazopata kila kukicha na muziki wake kuzidi kukubalika zaidi. Kwa hiyo tutegemee mengi kutoka kwake.
Post A Comment: