Yanga imemtwaa Kocha, Zahera Mwinyi Rais wa DR Congo ambaye tayari yupo nchini kukamilisha mazungumzo ya Yanga kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Kocha George Lwandamina ambaye ameshatimukia nyumbani kwao, Zambia.
Mmoja wa wanakamati wa Yanga, amesema kocha huyo alikuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo iliyokuja nchini kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars na kulala kwa mabao 2-0.
Kocha Mkuu wa DR Congo kwa sasa ni Florent Ibenge aliyewahi kuifundisha AS Vita, moja ya timu kubwa na kongwe nchini humo.
“Tayari ametua nchini jana, nafikiri atamalizana leo na uongozi tayari kwa kila kitu na ataanza kazi,” kilieleza chanzo.
Yanga ilikuwa chini ya Noel Mwandila na Shadrack Nsajigwa ambao walikuwa wakishikilia mikoba ya Lwandamina aliyeamua kurejea kwao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: