RAPA anayefanya vizuri kwa sasa kwenye gemu la Muziki wa Hip Hop Bongo, Awadhi Mtezo ‘Moni Central Zone’, amewaka kisa kuambiwa na mashabiki kwamba anategemea kiki kuusukuma muziki wake.
Akipiga stori na Star Showbiz, baada ya kuulizwa kuhusu komenti hizo za mashabiki kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, ambao walidai hivi karibuni alipokuwa anataka kupushi ngoma yake mpya ya Mwaah, alitumia kiki ya ugomvi na mwanamuziki Roma alifunguka hivi;
“Hata siku moja sitegemei kiki. Muziki wangu ni mzuri na unajiuza wenyewe. Kikubwa kilichokuwepo kwa sababu nilikuwa karibu na R.O.M.A, mambo yalikuwa hayaendi vizuri kwa sababu alikuwa anaonekana yeye tu na si mimi, lakini baada ya kila mtu kuchukua time yake, kwa sasa naonekana mwenyewe na si kwamba nategemea kiki!”
Post A Comment: