Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Katibu Mkuu wake, Charles Boniface Mkwasa umesema kuwa unatarajia kuwapatia wachezaji wake kifuta jacsho kwa kitendo cha kuwatoa Welayta Dicha FC ya Ethiopia na kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF).
Mkwasa amesema kuwa wanamshukuru Mungu kwa matokeo yale waliyopata na kuweza kusababisha wao kuweza kupita raundi hii na kwenda nyingine na kuahidi kuwapatia kifuta jasho wachezaji wao kwa kile walichokifanya.
Kwanza naweza kumshukuru Mungu kwa matokeo yale na kuweza kusababisha sisi kuweza kupita raundi hii na kwenda nyingine na pia nichukue nafasi hii kuwashuku kwa wachezaji na viongozi ambao wameambatana na timu na katika kuhamasisha pamoja na changamoto ambazo lakini wameweza kuonyesha umoja na kuweza kupata matokeo mazurili ili kuweza kuleta sifa kwenye nchi yetu.Tutaangalia wachezaji nao watapata kitu gani siwezi kuamua mimi peke yangu, lakini lazima tukae kama viongozi tuweze kuwazawadia wachezaji kile kitakachopatikana pia hizo fedha zitasaidia kuisaidia timu kwenye mzunguko wa pili, kutahitaji uangalifu mzuri kwa hizi fedha. Tutakaa na viongozi kupanga namna gani tuwazawadie wachezaji kama ‘bonus’ yao na pia kulipa matatizo madogo madogo ambayo tunaona tunaweza kuyalipa na kuyamaliza kwa wachezaji.
Baada ya kutinga hatua hiyo ya makundi kwa kuwatoa Welayta Dicha ugenini kwa jumla ya mabao 2 – 1, Yanga SC inatarajia kuvuna mgao wa Dola za Kimarekani laki mbili na elfu 75 ambazo ni karibia shilingi milioni 600 kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF).
Post A Comment: