Msanii wa Bongo Flava kwa sasa, Mimi Mars amefunguka kuhusu kurejea katika utangazaji wa TV.

Muimbaji huyo aliyekuwa akitangaza kipindi cha Weekend Gossip kupitia TV 1 amesema mipango ya kurejea katika utangazaji ipo ila bado ni vigumu kuweka wazi ni kipindi gani hasa.
“Mipango inafanyika kikubwa ni ku-keep up na mimi na watajua na watapata kusikia ni lini, wapi na sehemu gani,” Mimi Mars amesema
Katika hatua nyingine amezungumzia maisha ya muziki na yale ya utangazaji, utofauti upo wapi.
“Hamna utofauti kwa sababu kile kipindi watu walikuwa wanakifurahia, kusema kweli kile kipindi ndio kilinianzisha watu waweze kujua Mimi Mars ni nani na mashabiki wangu wengi nimewapata kupitia kipindi kile hadi nilipoingia kwenye muziki,” amesema.
Mimi Mars ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Papara’ ana historia yenye kushabiana na ile ya dada yake, Vanessa Mdee ambaye awali alikuwa mtangazaji wa MTV Base na Choice FM kabla ya kuingia katika muziki.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: