Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) amelalamikia kufinywa makalio na kiti alichokalia bungeni leo, hatua iliyomfanya kumwomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kuagiza ukarabati wa baadhi ya vifaa ndani ya Ukumbi wa Bunge hilo kwa kuwa asilimia kubwa ya viti vimechakaa.
Selasini ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma leo Aprili 30, wakati akiomba mwongozo kwa Spika baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.
“Mheshimiwa Spika watendaji wako wanakuangusha kwa sababu baadhi ya viti humu bungeni ni hatarishi, kwa mfano ninachokalia mimi leo kimenifinya kalio,” amesema Selasini na kusababisha wabunge na Spika kuangua vicheko.
Aidha akijibu mwongozo huo Spika Ndugai alimwambia suala hilo litachukuliwa hatua.
“Kuna watu wanauliza etu ni sehemu gani umefinywa… usijali mheshimiwa point noted,” alisema Ndugai.
Post A Comment: