Mwenyekiti
wa CHADEMA Taifa, Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa
Hai, Freeman Mbowet amempongeza Fatma Karume kwa kuchaguliwa kuwa Rais
mpya wa TLS.
“Ushindi
wako umetuma ujumbe kuwa mawakili wa Tanganyika wanajua msimamo wako na
wanaamini kwa dhati kuwa kwa kushirikiana na viongozi wenzako
mliochaguliwa kuongoza TLS utawavusha katika kipindi hiki ambacho Taifa
linapitia na kushuhudia majaribu mengi ya uvunjifu wa Katiba, sheria na
kanuni mbalimbali.
"Umepokea
kijiti katika wakati ambao mtangulizi wako (Tundu Lissu) yuko
hospitalini baada ya jaribio la shambulizi lililolenga kumuua
kushindikana.
“Tukutie
moyo kuwa CHADEMA kama taasisi ya kisiasa tukiwa wadau wa masuala ya
haki, sheria na utawala bora tuko nawe na tutaendelea kukupa ushirikiano
wakati wote wa uongozi wako, wewe na wenzako wote.” -Mbowe
Post A Comment: