Waziri wa Katiba na Sheria,  Palamagamba Kabudi ameikosoa kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kuwasaidia wanawake wenye watoto waliotelekezwa na waume zao  na kusema kwamba ilipaswa kufanyika kwa faragha.

Kabudi ametoa kauli hiyo leo Aprili 18, wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara hiyo baada ya mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kuhoji uhalali wa kampeni hiyo.

Profesa Kabudi amesema shughuli hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha kuwa inapaswa kufanyika kwa faragha si kama inavyofanyika sasa.

Wakati Kabudi akisema hayo, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amesema kampeni ya Makonda ni ishara ya kukosa kazi ya kufanya.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: