Hali
ni shwari mkoani Manyara. Hakuna dalili za maandamano. Hata hivyo
askari polisi wakiwa na magari, pikipiki na kutembelea kwa miguu
walionekana wakizunguka sehemu mbalimbali ili kuimarisha ulinzi.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP) Agustino Senga
akizungumza kwa njia ya simu leo Aprili 26, amesema mkoa huo upo
shwari kabisa.
Kamanda Senga amesema polisi wapo kwenye maeneo tofauti ya mkoa huo wakiendelea na kazi ya ulinzi wa raia na mali zao.
"Kwenye
mkoa wangu hakuna mtu aliyeandamana wala aliyehamasisha mtu kuandamana
wala hakuna aliyekamatwa juu ya hilo kwa kuhamasisha wala kuandamana,"
amesema kamanda Senga.
Mkuu
wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula akizungumza juu ya
maandamano hayo, aliwataka wananchi wenye nia hiyo kufanya shughuli zao
za maendeleo na kuachana na suala hilo.
"Kama
kuna mtu ana hoja yoyote aje mezani tuzungumze juu ya hoja yake na siyo
kutuletea habari za mambo ya kuandamana ambayo hayana tija yoyote kwa
jamii," amesema Mhandisi Chaula.
Post A Comment: