Soka ni burudani na siyo vita. Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara ametoa povu zito kutokana na kitendo cha beki wa Yanga Kevin Yondani kudaiwa kumtemea mate Asante Kwasi kwenye mchezo uliochezwa jana (Jumapili) katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yondani ameonekana kwenye vipande vya video akimtemea mate Kwasi wakati alipokuwa akimzuia kwenye goli la Yanga wakisubiri kupigwa kwa mpira wa kona.

Kupitia mtandao wa Instagram, Manara ameonyesha kukerwa zaidi na tukio hilo kitendo ambacho amemuahidi mchezaji wao Kwasi watalifanyia kazi kuhakikisha mambo kama hayo hayajirudii tena.

Huyu jamaa ni mshamba.mtu asiye na ustaarabu. bwege na hastahili kuachwa hv hv..ni tukio la hovyo zaid nchini kwa mwaka huu..nilikuwa namheshimu kama senior player ila kwa sasa namuona ni zaidi ya takataka..usela wa kihayawani..chuki hyo ya nn?nyie mmeshinda mara ngapi mbona hamjatemewa makohozi ?vtendo hv lazma vilaaniwe na kila mmoja…..kwasi nakuahidi hili jambo tutalisimamia kwa nguvu kubwa..na hongera kwa nidhamu wachezaji wetu…na lazma apimwe kama hana maradhi sugu ya kuambukiza huyu jamaa..na tunangoja kauli ya Yanga kwa ushenzi huu wa kipumbavu..samahani watu wangu kwa lugha kali..ila sina maneno laini ya kuelezea upumbav kama huu….bullshit!!!!!
Share To:

msumbanews

Post A Comment: