Mkoa wa Dar ea salaam leo hii (26 April 2018) umeadhimisha miaka 54 ya Muungano kwa kutoa misaada ya chakula na malazi kwa familia zilizoathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni.

Mkuu wa mkoa wa Dar Mhe. Paul Makonda amesema misaada iliyotolewa ni pamoja na Magodoro, Chandarua, Mashuka, Mito, Sukari, Unga,Mchele pamoja na Mafuta ya kupika.
RC Makonda amesema misaada hiyo itagawanywa kwa familia zaidi ya 600 zilizoathiriwa na mafuriko lengo likiwa ni kusaidia familia hizo ambazo zimekuwa zikiishi kwa tabu baada ya mvua kuharibu vyakula na mali.

Aidha RC Makonda amezishukuru taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center kwa kuamua kutumia maadhimisho ya muungano kugusa maisha ya familia zilizokuwa zikiishi kwa tabu.
Hata hivyo RC Makonda amesema kuwa Mkoa umeandaa mkakati wa kukabiliana na mafuriko ya Mara kwa Mara ambapo hivi karibuni atahitisha mkutano na wananchi wote waishio mabondeni ili kuangalia namna bora kutatua suala hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya Miraj Islamic Center Bwana Abdullah Mrus na Mwenyekiti wa taasisi ya Abdullah Aid Bwana Arif Ally Abdurahman kwa pamoja wamesema wameamua kutumia siku ya muungano kuzikumbuka na kusaidia familia ambazo zimekumbwa na mafuriko na sasa zinaishi kwa tabu.
Aidha wamempongeza Rais Dr. John Magufuli kwa kudumisha Amani na Mshikamano miongoni mwa Wananchi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: