Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemuwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC aliyemaliza muda wake kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda umefanyika hapa Luanda, leo tarehe 24 Aprili, 2018.

Mkutano huu umeitishwa baada ya mashauriano kati ya Mheshimiwa Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC na Mhe. João  Lourenço, Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikino ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC

Mkutano huu umetanguliwa na kikao cha Mawaziri ambacho kilifanyika jana tarehe 23 April 2018.

Mkutano huu ulihusisha nchi wanachama sita tu wa SADC Double Troika na Viongozi wafuatao walihudhuria,

Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço  , Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation),Mhe. Hage Geingob, Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit, Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia na Makamu Mwenyekiti wa SADC Organ, Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland na Mwenyekiti wa Summit anayetoka;

Mheshimiwa Joseph Kabila Kabange, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho walialikwa na walihudhuria.

Mkutano huu utapitia na kujadili ajenda zifuatazo:-
  1.  Hali ya siasa na usalama katika Falme ya Lesotho;
  2.  Hali ya siasa ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo;
  3. Hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Madagascar; na
  4. Masuala ya demokrasia katika kanda ( Consolidation of Democracy in the region)
KUHUSU HALI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA NCHINI LESOHO:-
  1. Mkutano huu umevitaka  Vyama vyote vya Siasa kulipa uzito suala la Mjadala wa Kisiasa na Mchakato wa Mageuzi ya Kisekta na kushiriki kikamilifu kwenye michakato yote ili kupata suluhisho la kudumu katika changamoto za kiusalama na kisiasa;
  2. Pia Mkutano huu umeitaka Serikali ya Lesotho na wadau wengine kukamilisha mjadala wa kitaifa ifikapo mwezi Juni, 2018 na kutoa taarifa kwenye kikao kijacho cha kawaida cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC ambacho kimepangwa kufanyika Augosti, 2018;
  3. Pia Misheni ya Ulinzi nchini Lesotho (SADC Preventive Mission in the Kingdom of Lesotho – SAPMIL ) imeongezewa muda kwa kipindi kingine cha miezi sita kuanzia Mei 20, 2018.
KUHUSU  HALI YA SIASA, ULINZI  NA USALAMA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA    KONGO (DRC)

Nchi wanachama zitaombwa kuisaidia Jamhuri  ya Kidemokrasia ya   Kongo (DRC)  kwenye kipindi hiki wanachoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu kwa lengo la kuhakikisha kuwa uchaguzi huu unafanyika katika mazingira ya amani.

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huu ulitumia fursa hiyo kuomba nchi wanachama wa SADC kumuunga mkono Mheshimiwa Stephen Maselle ( Mb), ambaye anawania  nafasi ya Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika ( Deputy President of the Pan African Parliament).
Share To:

msumbanews

Post A Comment: