Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
jana amkutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa
nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt .
Makamu
wa Rais yupo nchini Uingereza kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa
Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) akimwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli.
Katika
mkutano wake na Waziri huyo wa Uingereza Makamu wa Rais alielezea hatua
kubwa iliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika Elimu mara baada
ya kuamua Elimu iwe bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.
Pia
Makamu wa Rais alishukuru mradi wa DFID unatekelezwa mkani Simiyu na
kuomba mradi huo uongezewe maeneo ili uweze kuwanufanisha watoto wengi
wa kike.
Makamu
wa Rais pia alizungumzia namna Majukwaa ya Kuwawezesha wanawake
kiuchumi yanavyofanya kazi huku taratibu mbali mbali zinafanyika ili
mabenki yaweze toa mikopo kwa riba nafuu.
Mwisho
Makamu wa Rais alizungumzia jitihada mbali mbali zinazofanywa na
Serikali katika kuboresha Mazingira ya kufanya Biashara nchini.
Naye
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt
ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada wanazofanya katika
kuboresha huduma za kijamii, alisema nchi yake ipo tayari kusaidia
katika masuala ya makusanyo ya kodi, kuboresha uwezo wa walimu kwa
kuwapatia mafunzo mbali mbali.
Post A Comment: