Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu imeitaka Tanzania kumrejesha nchini Anudo Ochieng Anudo aliyevuliwa uraia wa Tanzania na kuhamishiwa Kenya ambapo pia hakupokelewa.
Kufuatia hatua hiyo, Anudo alibaki katika eneo ambalo halipo chini ya nchi yoyote (no man's land) katikati ya mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Sirari.
Mahakama hiyo chini ya Rais wake, Sylvain Ore imesema, Tanzania ilikiuka sheria za kimataifa kwa kumfukuza mtuhumiwa pasi na kumpa nafasi ya kusikilizwa.
Mahakama imeamuru Tanzania kuchukua hatua stahiki kumrejesha Anudo nchini, kuhakikisha anakuwa salama na kisha ipeleke ripoti katika mahakama hiyo ndani ya siku 45.
Post A Comment: