Mbunge
wa jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh.
Ridhiwani Kikwete amefunguka na kusema kitendo cha polisi mwenye namba
E1156 Koplo William Marwa ambaye anadaiwa kufanya mauaji kwa mdogo wa
Heche kimemsikitisha sana.
Ridhiwani
amefunguka hayo baada ya Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Tarime na
Rorya kudai kuwa linamshikilia polisi huyo kwa tuhuma za kumchoma kisu
Bwana Chacha Heche Suguta ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Tarime Vijijini
John Heche.
"Kitendo
kilichotokea sio tu kimesikitisha ukoo wa Bwana Heche lakini kwangu
binafsi. Jeshi letu limetengenezwa kulinda watu na mali zao sio kuumiza
wasio na hatia. Ni imani yangu Serikali itasimamia haki kwa familia ya
Heche. Poleni sana kwa msiba. Mungu awape subira John Heche" alisema
Ridhiwani
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, Henry Mwaibambe amethibitisha
kumshikilia askari wake mwenye namba E1156 Koplo William Marwa kwa
tuhuma za kusababisha kifo cha kijana Saguta Chacha mwenye umri wa miaka
26 mkazi wa Sirari wilayani Tarime mkoani Mara kwa kumchoma Kisu.
Post A Comment: