Mara baada ya wachezaji riadha wa Tanzania kuambulia patupu kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola huko nchini Australia, Katibu Mkuu wa mchezo huo hapa nchini, Wilhelm Gidabuday amesema kuwa kukosa Medali kwa wachezaji wetu ni jambo la kujitakia na kamwe haliwezi kumnyima usingizi.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini ( RT ), Wilhelm Gidabuday
Gidabuday ambaye licha ya kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini ( RT ) lakini pia ni mwanariadha aliyewahi kuiletea sifa kubwa Taifa miaka ya 80 ameyasema hayo kupitia kipindi cha michezo cha Radio Magic FM.
“Kama tumeshindwa basi tuhesabu miaka minne mbele kwa sababu jana wakati wanafunga mashindano kijiti walipewa Uingereza kwa hivyo tujipange kufanya vizuri huko kama tutakuwa tumejirekebisha,”amesema Gidabuday.
“Nahaya ni mashindano makubwa Serikali inahusika na ndiyomaana mkuu wa msafara lazima awe mtu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kwasafari hii alikuwa ni Mkurugenzi wa Michezo ambaye anawakilisha serikali sasa kama kunaumuhimu huo wa sisi kupata medali watu hawakupiga kelele , ruhusa za wanariadha zilivyokosekana ulimsikia nani mwingine aliyepiga kelele na kulalamika na kusikia uchungu kwamba kwa nini wanariadha wetu wamenyimwa ruhusa nani mwingine ulimsikia kama siyo mimi peke yangu.”
“Tunaimba tunataka medali lakini wengine hawataki medali, hivyo sisi tumeshindwa na mimi sikosi usingizi kwasababu siyo tumeshindwa kwakukaa tu nakulala hapana tulifanya majukumu yetu yote ni sawa na timu yetu ya Taifa asipokuwepo Samatta au wachezaji wengine wakali unategemea ushindi .”
Post A Comment: