STAA wa Hip Hop kutoka Marekani, Kanye West, hivi karibuni kupitia ukurasa wake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Twitter, aliamua kumrusha mwanamuziki anayechipukia kutoka Bongo, anayejulikana kwa jina la Lo Sayaloha Ski, akimpa pongezi kutokana na wimbo wake mpya uitwao iBeen.
Kanye alimrusha Ski, baada ya ‘kumtag’ wimbo wake huo katika Mtandao wa Twitter na Kanye akimrusha aliandika maneno yaliyosomeka ‘Lo SayAloha Ski is a musical GENIUS #ibeen’.
Baada ya posti hiyo mastaa mbalimbali wa Hip Hop Bongo, akiwemo G Nako walimpongeza mwanamuziki huyo na kumwambia azidi kukaza kamba afike mbali zaidi.
Post A Comment: