Kamati ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii imeuponda utaratibu unaotumika na Serikali wa kufungia nyimbo za wasanii, zisizoendana na maadili ya kitanzania kwa maelezo kuwa unaleta changamoto kwa wasanii.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwaka 2018/19 kwa niaba ya mwenyekiti wake Peter Serukamba, mbunge wa Ludewa (CCM), Deogratius Ngalawa amesema vyombo vinavyohusika na usimamizi vinapaswa kuhakikisha vinatimiza majukumu yake kwa kukagua nyimbo zote za wasanii kabla hazijatoka.

“Lengo ni kuhakikisha hakuna wimbo unaotoka kama haujazingatia maadili. Kuangalia nyimbo ambazo ni za kimataifa na kuzipa kibali maalum kwa maana ya muda na mahali pa kuutumia wimbo huo kabla haujaanza kutumiwa na vyombo vya habari.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: