Leo ni vita ya walima miwa mkoani Kagera inafanyika ambapo wenyeji Kagera Sugar watakuwa wana kibarua cha ligi kuu dhidi ya mtibwa Sugar.

Kagera ambayo imekuwa haina maendeleo mazuri msimu huu itakuwa inapigana kufa kupona kutafuta matokeo ya kuifanya iendelee kusalia katika ligi.

Katika msimamo wa ligi inaonesha imekamata nafasi ya 14 ikiwa imejikusanyia alama 23 ambazo ni tofauti na Mtibwa iliyoshika nafasi ya 6 ikiwa na pointi 33.

Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: