Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limewatia nguvuni watu watatu kwa wizi wa vyombo vya muziki na viti makanisani mkoani humo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, Mbeya watu hao ni William Sanke (23) mkazi wa Isanga, Eliudi Mwansule (28) mkazi wa Mwakibete Viwandani na Noa Molela (26) mkazi wa Mama John.
Misako iliyofanyika imefanikisha kupatikana kwa mali mbalimbali za wizi ambazo ni spika kubwa 15 za aina mbalimbali, mixer nane, amplifier moja, viti vya plastic 108 vya rangi mbalimbali.
Baada ya kukamatwa na kuhojiwa, watuhumiwa walikiri kuhusika katika matukio ya kuvunja na kuiba Makanisani nyakati mbalimbali na mara baada ya kuiba mali hizo huwapelekea wauzaji ambao pia wamekamatwa.
Watuhumiwa wote wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Post A Comment: