Na George Mganga

Afisa Habari wa zamani wa klabu ya Yanga, Jerry Muro, ameipongeza Simba kwa ushindi ilioupata dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu bara uliopigwa Jumapili ya Aprili 29 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Erasto Nyoni kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Shiza Kichuya katika dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza.

Muro amewapongeza Simba huku akimsifu Ofisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara kwa kuwahamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi Uwanjani ili kuipa timu yao hamasa.

Mbali na hayo, Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Muro amewapa pole Wanayanga wote kwa ujumla huku akiwaomba waige mfano kwa Simba namna walivyojitoa kuhamasisha mashabiki wao kujitokeza kwa wingi uwanjani.




Muro ameeleza hayo akiamini kuwa shabiki ni mchezaji namba 12 hivyo anapokuwepo Uwanjani hutoa motisha nzuri kwa wachezaji ili wapate morali ya kujituma.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: