Muigizaji
wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka mazito kwa mumewe staa wa Bongo
fleva Dogo Janja ambapo amedai kuwa ni moyo wake na kukiri kuwashangaa
watu wanaosema yeye ni mdogo.
Ndoa
ya Dogo Janja na Irene Uwoya ilishangaza watu wengi ilipofungwa mwaka
jana mpaka hivi sasa kuna watu ambao hawaamini kuwa wawili hao wameoana.
Na
imekuwa ngumu kwa watu wengi kuzoea Mahusiano hayo hasa kwa sababu
tofauti kubwa iliyopo baina yao kuanzia umri mpaka vitu vingine ambavyo
vinaonekana baina yao.
Lakini
kadri siku zinavyozidi kuenda wapendanao hao wameendelea kuuthibitishia
uma wa Watanzania kuwa wanapendana na watazidi kuwa pamoja.
Kupitia
ukurasa wake wa Instagram Uwoya kamfungukia mazito mumewe Dogo Janja
ambapo amekiri kuwa anampenda mumewe na kusema anawashangaa watu ambao
wanekazana kumsema ni mdogo kwani yeye anamuona mtu mwenye akili sana:
"Nakupenda
sana sijawahi kukutana na mwanaume mwenye akili kama wewe na muelewa
kama wewe….mdogo lakini mmmnh mimi ndio ninajua ndio maana wakiongea
nawaangalia tu nasema iiiiii Dogo Janja wewe ndiye moyo wangu”.
Dogo
Janja naye anaonekana amekolea na penzi la Irene kwani mara kwa mara
anamposti mkewe na kumwagia sifa lukuki kama mke mwema na mwaminifu na
kadhalika.
Post A Comment: