Kiungo Andres Iniesta amemwaga chozi mbele ya watoto, mke wake na wachezaji wenzake wa FC Barcelona.

Iniesta amemwaga chozi wakati akiaga mbele yao baada ya kuichezea Barcelona kwa miaka 22, sasa anastaafu.

Anaondoka Barcelona aliyojiunga nayo mwaka 1996 akiwa mtoto baada ya kuisaidia kubeba makombe 31 sawa na Lionel Messi.

Amekataa kwamba atajiunga na Manchester City au klabu nyingine ya Ulaya na taarifa zimeeleza anakwenda kucheza Ligi Kuu China.

Alijiunga Barcelona akiwa na umri wa miaka 12 na mwisho akageuka kuwa tegemeo na baadaye shujaa wa klabu hiyo maarufu duniani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: