Kifungu cha 43 cha Police Force and Auxiliary Services Act, kinasema mtu yeyote anayetaka kukusanya(collecting), kufanya(forming) au kuandaa(organising) mkusanyiko au matembezi(procession) kwenye eneo la umma atawasilisha taarifa kwa maandishi sio chini ya masaa arobaini na nane (48) kabla ya mkusanyiko au matembezi hayo kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi wa eneo hilo akitaja;
a) sehemu na muda
b) sababu za mkusanyiko
c) mambo mengine kama itakavyokuwa imeelekezwa na Waziri na kuchapishwa kwenye Gazette la Serikali

Taarifa hiyo ikishatolewa aliyeitoa anaweza kuendelea isipokuwa tu kama atapokea AMRI kutoka kwa polisi ikimzuia kufanya hivyo.

Polisi hapaswi kuzuia mkusanyiko au matembezi hayo mpaka ajiridhishe kwamba hayatavunja amani au kuathiri utulivu wa umma au kusimamia usalama au hayatatumika kwa sababu nyingine ya uvunjifu wa sheria.

Kifungu hiki kinahusu mkusanyiko au matembezi ambayo yameandaliwa na mtu yeyote sio lazima kiwe chama cha siasa.

Sasa kesho kabla ya kuitikia wito wa kuandamana jiridhishe kuhusu yafuatayo;
1. Nani ametoa taarifa ya mkusanyiko au matembezi ya amani?
2. Taarifa hiyo imetolewa wapi na ndani ya muda gani?
3. Polisi wameipokea taarifa hiyo?
4. Je hakuna AMRI ya kuzuia?
5. Sababu ya wewe kwenda huko (hii sio sheria)

Kama ukijiridhisha unaweza kutoka nyumbani ukaenda eneo ambalo taarifa imetolewa. Kama hayo hayajafanyika basi ujue unavunja sheria na ni kosa la jinai.

Tambua kwamba polisi wana mamlaka kamili kuzuia mkusanyiko na matembezi yoyote ambayo ni kinyume cha sheria. Na ikiwalazimu kutumia nguvu watatumia bila kuvunja sheria.

Mwisho, kibali cha kukusanyika kilichotolewa Sweden, London au Marekani hakina nguvu ya kisheria Tanzania. Kama kibali kimetolewa huko unapaswa ujiulize kwa nini kiliombwa na kutolewa. Na kwa nini hapa hakijaombwa!!

Ni haki yako kufuata mkumbo na kushabikia jambo lolote hata kama ni la kipuuzi. Hiyo ndio demokrasia na uhuru wa kuchagua. Hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine inapokuja suala la kuchagua. Usimpangie mtu. Anayetaka kwenda na aende.

Alberto Msando
Dar Es Salaam
25.04.07
Share To:

msumbanews

Post A Comment: