Baada ya Arsene Wenger kutangaza rasmi kuacha kuifundisha Arsenal mwishoni mwa msimu huu, fahamu makombe ambayo kocha huyo ameyachukua katika miaka yake 22 aliyokuwa akifundisha timu hiyo.
Katika miaka hiyo 22 ndani ya klabu hiyo ya Uingereza, Wenger amefanikiwa kushinda jumla ya makombe 17 huku akiisimamia Arsenal ikicheza jumla ya michezo 1,228 chini yake.
Katika michezo hiyo ambayo Arsenal imecheza mpaka sasa, Wenger amefanikiwa kuibuka na ushindi wa michezo 704.
Wenger amefanikiwa kushinda makombe matatu ya ligi kuu Uingereza mwaka 1997–98, 2001–02 na 2003–04.
Wakati huo huo amefanikiwa kushinda makombe saba ya FA ikiwa ni mwaka 1997–98, 2001–02, 2002–03, 2004–05, 2013–14, 2014–15 na 2016–17. Pia ameshinda makombe saba ya Community Shields (1998, 1999, 2002, 2004, 2014, 2015 na 2017).
Lakini kubwa zaidi linalokumbukwa kwa mzee Wenger ni katika msimu wa 2003–04 alipoiwezesha Arsenal kushinda taji la ligi kuu Uingereza bila ya kufungwa mechi hata moja huku ikishinda michezo 27 kati ya 38 waliocheza na kutoa sare michezo 11.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: