Hali
ya usalama mkoani Iringa leo imeendelea kuwa shwari licha ya tishio la
maandamano yaliyotarajiwa kuwepo huku ulinzi ukiimarishwa katika baadhi
ya maeneo yenye mkusanyiko mikubwa kama benki na vyuo vikuu.
Hata
hivyo, Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia kwa mahojiano Diwani
wa Kata ya Igumbiro, Musa Mlawa kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio
halali.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire Diwani huyo
anashikiliwa kwa mahojiano ili kubaini chanzo cha mkusanyiko huo.
Ulinzi
mkubwa ulionekana kuimarishwa sana katika lango la kuingilia Chuo cha
Kikatoliki ha Ruaha (RUCU) ambacho kinapakana na Benki ya NMB Tawi la
Mkwawa.
Katika
Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa na Chuo cha Elimu Mkwawa hali ilikuwa
shwari na ilionekana gari moja tu ikipiga doria ikiwa na askari wachache
ikizunguka maeneo tofauti tofauti ya mji wa Iringa.
Post A Comment: