Simba ilipata penati mnamo dakika ya 80 kwa John Bocco kuchezewa madhambi na Mwamuzi wa mchezo kuamuru penati hiyo ipigwe kuelekea lango la Prisons.
Manara amewaita ni wanafiki huku akieleza kuwa kuwa wamekuwa wakiiandama Simba kila siku pale inapotokea inastahili kupewa haki yake Uwanjani.
Mkuu huyo wa kitengo ameeleza baadhi ya wadau na wale wote waliopinga penati hiyo, wamekuwa wakiisema Simba vibaya pale inapotokea imefanyiwa sivyo Uwanjani na badala yake wanashindwa kuitetea.
Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mcheo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa huku magoli yakifungwa na Bocco pamoja Emmanuel Okwi.
Post A Comment: