Msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kwa Jina la usanii kama Gigy Money aliyetamba na kibao chake cha Nampa papa amehofia kupotezwa katika gemu ya Bongo fleva kipindi hiki ambacho ni mjamzito.

Gigy Money ameibuka baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu huku hali hiyo Ikiwa imesababishwa na kuwa mjamzito hivyo kukiri kuwa anashindwa kufanya kazi nyingi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy Money ameongelea hofu yake ya kusahaulika kutokana na kuwa kimya na kuandika ujumbe mfupi uliosindikizwa na picha zake mpya:

"Hapa mjini nikisema siposti msije mkanisahau bure nipo kiranja wa mashangingi hali ni mbayaaa hali ni teteee”.

A
Share To:

msumbanews

Post A Comment: