Msanii Dogo Janja ambaye anaendelea kutrend kwenye mitandao baada ya ndoa yake na muigizaji wa filamu bongo Irene Uwoya, amewataka wanawake kuwa makini na wanaume kwani ni watu ambao sio wakweli kabisa.

Akizungumza kwenye kipindi cha DADAZ kinachorushwa na East Africa Television, Dogo Janja amesema wanaume wengi hutumia uongo ili kuwanasa wanawake, hata kufikia hatua ya kujitangazia mali ambazo hana uwezo wa kumiliki.

“Unajua vijana wengi kwenye mapenzi ni waongo, hususan wanaume ni waongo sana, ogopa sana yule mwanaume ambaye anakufuata na magari, heshimu yule anayekufuata na mguu anakanyagia, yuko real, anakueleza mimi nakupenda, uwezo wangu mimi ni hivi, huenda nikapata huenda nikakosa, tofauti na yule anakuja anakuchukua anakupeleka huku, anakununulia wigi la laki nane, mwisho ataanza kukopa kopa atakuongopea”, amesema Dogo Janja.

Dogo Janja amesema hata yeye moja ya kigezo cha kumpata mke wake ambaye ni mmoja ya waigizaji warembo bongo, alikuwa muwazi na mkweli, na kumwambia kabisa hana uwezo mkubwa kipesa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: