Mkuu wa wilaya ya Monduli Mh.Idd Hassan Kimanta Pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama Wametembelea Eneo la Mto wa Mbu ambalo limekumbwa na Mafuriko Makubwa yaliosababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.Mvua hizo zimeleta athari kubwa ikiwepo kuharibu mali na kuleta adha kwa wananchi.

Maeneo yaliokubwa na adha mafuriko hayo ni Komwex,Kisutu,Jangwani na Migombani.

Mkuu wa Wilaya alishiriki kufanya usafi katika daraja kubwa ambalo huziba kutokana na uchafu migomba na kusababisha kubadilisha mwelekeo wa Maji na kuelekea katika nyumba za wananchi.


Jitihada za haraka zimechukuliwa na mkuu wa wilaya ikiwa ni kufanya tathmini ya kuongeza matoleo ya maji ili kupunguza athari za mafuriko hayo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: