Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro amefungua na
kuongoza mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
mkoani Shinyanga uliolenga kujadili namna ya kufanikisha zoezi la chanjo
hiyo kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 mkoani humo.
Mkutano
huo umefanyika leo Jumanne Aprili 17,2018 katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa
chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga.
Akifungua
mkutano huo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya
mkuu wa mkoa wa Shinyanga alisema Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa chanjo imeanzisha
chanjo mpya ya kuwakinga na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kwa
wasichana wenye umri wa miaka 14.
Matiro
alisema saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza nchini Tanzania kwa
kusababisha vifo ikifuatiwa na saratani ya matiti ambazo zote
zinasababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akina mama
vitokanavyo na saratani hivyo kunahitajika juhudi na ushirikiano zaidi
kupunguza vifo hivyo.
“Lengo
la kuanzisha chanjo hii ni kukinga mabinti kutokana na madhara makubwa
yanayoweza kuwapata ambayo husababisha vifo vingi kwa wanawake,na
walengwa wa chanjo hii mwaka huu ni wasichana wote wanaotimiza miaka 14
ambapo katika mkoa wa Shinyanga wasichana wasiopungua 29,479
watachanjwa”,aliongeza.
Alisema
chanjo hiyo itatolewa bila malipo katika vituo vya kutolea huduma vya
serikali na binafsi ,baadhi ya shule na maeneo katika jamii ambazo
zitatolewa kwa njia ya huduma za mkoba.
“Saratani
hii inachangiwa na vitu vingi ikwemo kuanza kujamiiana katika umri
mdogo,kuwa na wapenzi wengi,ndoa za mitaala,kuzaa watoto wengi na
uvutaji wa sigara”,alieleza.
Alizitaja
dalili za saratani ya mlango wa kizazi kuwa ni kutokwa damu ya hedhi
bila mpangilio,kutokwa damu baada ya kujamiiana,maumivu ya mgongo,miguu
na kiuno,kuchoka,kupungua uzito,kukosa hamu ya kula,kutokwa uchafu wa
rangi ya kahawia au wenye damu kwenye uke na maumivu ya miguu au
kuvimba.Hata
hivyo alisema dalili mbaya zaidi zinazoweza kujitokeza kuwa ni pamoja
na kuishiwa damu,figo kushindwa kufanya kazi,kupatwa na fistula na
uvimbe wa tezi.
Kwa
upande Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume alisema kati
ya wasichana 7304 wanaougua saratani ya mlango wa kizazi nchini kila
mwaka,4216 sawa na asilimia 58 wanafariki dunia hivyo ni muhimu zaidi
kupata kinga kuliko tiba. Alisema
uzinduzi rasmi wa chanjo hiyo mkoani Shinyanga utazinduliwa siku ya
Jumatatu Aprili 23,2018 katika manispaa ya Shinyanga.
Naye
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela alisema tayari pesa kwa
ajili ya chanjo hiyo zimeshatumwa kwenye halmashauri kinachotakiwa ni
utekelezaji tu ili kuhakikisha mkoa unafanya vizuri katika zoezi hilo la
utoaji chanjo kwa wasichana.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua mkutano wa wadau wa
chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga
Matiro
alisema serikali imeamua kuanza kutoa chanjo ya saratani ya mlango wa
kizazi kwa sababu saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa
kuua wanawake wengi ukilinganisha na saratani nyingine nchini.
Mganga
mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akizungumza wakati wa
mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani
Shinyanga.
Katibu
Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza wakati wa mkutano
wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga.
Mkutano ukiendelea.
Wadau wakiwa ukumbini..Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba na Afisa Tawala wilaya ya Kahama, Said Yasin
Kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngassa Mboje akiwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bakari Kasinyo
Wadau wakiwa ukumbini
Mkutano unaendelea.
Mtakwimu (Mpango wa taifa wa chanjo), David Kayabu akitoa mada kuhusu zoezi la chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
Daktari
wa Meno mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya ambaye ni Mkufukunzi wa
mafunzo ya chanjo ya HPV akitoa mada ukumbini kuhusu chanjo hiyo
Picha za pamoja wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
Picha za pamoja wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
Picha za pamoja wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
Picha za pamoja wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.
Post A Comment: