Na George Mganga
Wakati kikosi cha Yanga kikiondoka alfajiri ya leo kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaita Dicha FC, Ibrahim Ajibu na Andrew Vincent 'Dant, ni miongoni mwa wachezaji waliosalia Dar es Salaam.
Wachezaji hao wameshindwa kuungana na kikosi hicho kutokana na kukumbwa na majeraha hivyo kushindwa kusafiri na timu.
Dante aliumia katika mchezo wa kwanza dhidi ya Waethiopia uliopigwa Uwanja wa Taifa na kumfanya akosekane Uwanjani dhidi ya Singida United.
Ajibu na Dante watakuwa wanapata matibabu ili kuwa fiti kuelekea mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba SC itakayopigwa Aprili 29 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kushindwa kujumuika na wenzao katika safari ya Ehtiopia, kunawapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea pambano hilo ambalo huteka hisia za wadau na mashabiki wengi wa soka la hapa Tanzania.
Said Mussa pamoja na Ramadhani Kabwili, nao wamesalia nchini kwa majukumu ya kuitumikia Ngorongoro Heroes ambayo inajiandaa na mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON dhidi ya Congo.
Post A Comment: