Bunge limeitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kufanya ukaguzi polisi, magerezani na sehemu nyingine zinazolalamikiwa kuvunja haki za binadamu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa, alisema hayo Jumatano Aprili 18, wakati akisoma maoni ya kamati yake kwenye mapato na Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria.
“Kwa kuwa kumekuwapo na malalamiko mengi kuhusu uvunjwaji wa haki za binadamu, ukiukwaji wa misingi kuhusu utawala bora nchini pamoja na tuhuma za kushikiliwa watu magerezani, polisi na sehemu nyinginezo nchini, pasipokuwepo utoaji haki au majibu yanayoridhisha.
“Kamati inashauri tume ifanye ukaguzi katika sehemu zote nchini zenye malalamiko hayo na kutoa taarifa kwa mujibu wa sheria ili kutatua changamoto hizo endapo zitabainika kuwepo,” alisma Mchengerwa.
Kamati hiyo pia ilishauri Tume ya Utumishi wa Mahakama, kutatua changamoto ya mahakimu na kuhamishwa vituo na kupandishwa vyeo bila kulipwa stahiki zao kwa wakati.
Kwa upande wa Kamati ya Bajeti, Mchengerwa amesema kati ya fedha zinazoombwa kwa mwaka 2018/19, ikilingishwa na zile za 2017/18, matumizi mengineyo zimeongezeka kwa asilimia moja, za maendeleo zimeongezeka kwa asilimia 98 huku za mishahara zikipungua kwa asilimia 3.3.
Post A Comment: