Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli wamejiuzulu nafasi zao mapema leo Aprili 30 2018.
Madiwani waliojiuzulu ni Diwani wa kata ya Meserani Ndg. Lothi N Mollel, na Diwani wa kata ya Lolkisale Ndg. Solomon K Mollel madiwani hawa wote wamejiuzulu nafasi zao zote ndani ya Chadema na Kujiunga na Chama cha Mapinduzi Ccm na kufanya hadi sasa ndani ya Wilaya ya Monduli kufikia Madiwani Saba waliojiuzulu ndani ya saa 72.
Post A Comment: