Pia Mwakyembe amesema imebidi mwanamuziki Faustina Charles ‘Nandy’ naye akamatwe kisha kuhojiwa na wanaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani.
Mwakyembe ametoa wito kwa vijana kuwa mitandao si kokoro la kupeleka uchafu wote ambao umezuiwa na sheria na kwamba nchi ina utamaduni wake ambapo inahitajika kulinda kizazi cha sasa na cha kesho.
Waziri Mwakyembe amesema “Tulitunga sheria mwaka 2010 lakini tulikosa kanuni za kuweza kubana hasa maudhui upande wa mitandao, tumeshatunga hizo kanuni na sasa hivi hizo kanuni zimeanza kufanya kazi. Kuna baadhi ya wasanii wetu ambao walianza kufanya uhuni uhuni ndani ya mitandao ya kijamii jana tumeweza kumkamata msanii nyota Tanzania Diamond na tumemfikisha polisi na anahojiwa kutokana na picha chafu alizozirusha vile vile inabidi hata binti Nandy naye akamatwe ahojiwe,“amesema Waziri Mwakyembe.
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba Newsili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.
Tumekurahisishia;
Post A Comment: