SERIKALI imezindua mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kemikali za kutengeneza dawa za kusafishia maji kitakachogharimu sh. Bilioni 256.
Uzinduzi huo umefanyika eneo la Mlandizi Msufini mkoani Pwani jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samiah Suluhu Hassan.
Mwijage alisema mradi huo ukikamilika utasaidia serikali kuokoa kiasi cha fedha kilochokuwa kikitumika kununua dawa hiyo nje za nchi.
” Mradi huo ni wa tatu kwa ukubwa Afrika na kwa sasa tunatarajia kuzindua viwanda vingine tisa vilivyo na viwango. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Na ili kuhakikisha adhma ya viwanda inafanikiwa nitatoa eneo langu kwa ajili kujenga jumba la utamaduni wa viwanda, ” alisema.
Mwijage aliwataka Watanzania kujenga uthubutu wa kuwekeza kwenye viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi.
4Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Justine Lumbert , alimwakikishia Rais Dk.John Magufuli kuwa anacho kikosi mahiri nchini kwa ajili ya jenzi wa viwanda kwa mkoa wa Pwani.
Alisema mradi huo wa dawa ni mkubwa barani Afrika hivyo utaisaidia nchi kutengeneza aina ya dawa ya Chlorine itakakayotumika kusafisha maji.
” Utengenezaji wa dawa hiyo hutumia chumvi, sasa hakuna chumvi yoyote itakayouzwa nje ya nchi hadi mahitaji ya kiwanda hicho yatakapojitosheleza kwa sababu bidhaa zitakazotengenezwa zitakuwa na soko la asilimia 20 ndani ya nchi na 80 nje ya nchi,” alisema.
Mkurugenzi huyo ujenzi wa mradi huo utagharimu kiasi cha sh. Bilioni 256 kwa eneo la hekari nane na utakamilika ndani ya miezi 23.
” Tunaiomba serikali kuweka sheria na kanuni stahiki zitakazosaidia kulinda bidhaa na malighafi ya chumvi itakayotumiwa na mradi huu,” alisema.
Lumbert alitaja faida za mradi huo, utasaidia kuingizia taifa fedha za kigeni, kuokoa fedha za kununulia dawa nje, kuokoa gharama za matumizi ya kusafisha maji nchini na kuongeza ajira rasmi kwa vijana takribani 700.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe, alimuagiza Mkurugezi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja, ndani ya siku tatu anakutana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo kwa ajili ya ujenzi wa pipa kubwa la maji eneo la Mlandizi ili kuhakikisha yanapatikana eneo hilo kwa urahisi.
” Kwa Wizara yangu itabadilisha muundo wa ununuzi kwani tutakuwa tukinunua ununuzi wa pamoja kuanzia Julai mwaka huu sasa wizara yangu haitakwenda kununua sawa ya kusafisha maji nje wakati itakuwa ikipatikana nchini,” alisema.
Kamwele alizitaja aina ya upungufu uliokuwepo katika wizara yake kuwa ni utengenezaji wa mabomba ya chuma cha pua na dawa ya kusafisha maji kwa haraka iliyo na uwezo wa kuzamisha vumbi na matope kwa haraka.
Naye Mhandisi Ndikilo alisema mradi wa kiwanda hicho ni wa tofauti Afrika Mashariki kwa sababu Afrika kinapatikana nchi ya Misri na Nigeria.
” Wawekezaji tambueni ya kuwa mkoa wa Pwani uko salama kwa hiyo msipigiwe kelele na mitandao ya kijamii.
“Kiwanda hicho kinahitaji tani 2500 ya chumvi kwa mwezi kwa hiyo wazalishaji changamkieni fursa hiyo kwa sababu hakuna chumvi itakayochukuluwa nje ya nchi,” alisema.
Post A Comment: