Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya Commerial Bank of Africa (CBA) Tanzania, Gift Shoko akizungumza na wadau wa benki hiyo katika hafla fupi ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo katika hoteli ya Mt. Meru jijini Arusha, huku akiwajulisha hatua mbalimbali za kibenki zilizoboreshwa kwa wateja wao (Habari picha na Pamela Mollel Arusha)
Wadau wa benki ya Commerial Bank of Africa,CBA wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Arusha kwa lengo la kuwajulisha hatua mbalimbali walizozifikia huku wateja wao wakipata wasaa wa kueleza changamoto zinazowakabili.
Mkurugenzi Mkuu Mendaji wa Be Gift Shoko kushoto akizungumza na mmoja wa wadau wa benki hiyo jijini Arusha
Mkuu wa Idara ya Masoko wa benki ya CBA, Julius Konyani akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni na wadau wa benki hiyo jijini Arusha kwa lengo la kuwajulisha hatua mbalimbali walizozifikia huku wateja wao wakipata wasaa wa kueleza changamoto zinazowakabili.
Wadau wa benki hiyo wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni jijini Arusha
Na Pamela Mollel,Arusha
UKATA wa fedha katika uwekezaji na kukuza biashara ya utalii mkoani hapa umepata tiba baada ya Commerial Bank of Africa, kusema itashirikiana na wafanyabiashara kuwapa mikopo hadi kufikia dola za Marekani milioni 50 kwa atakayetaka.
Mkuu wa Idara ya Masoko wa benki hiyo, Julius Konyani, alisema wafanyabiashara 500 katika sekta ya utalii mkoani hapa kila mmoja anaweza kukopeshwa dola za Marekani milioni 50.
Alisema hayo katika ya katika chakula cha jioni walichoandaa kwa ajili ya kubadilishana nao mawazo na wateja wao.
“Mteja mmoja anaweza kukopeshwa dola za Marekani milioni 50, tunaweza kuwakopesha wateja 500 hapa Arusha kila mmoja kiasi hicho cha mkopo hapa,” alisema.
Alisema benki yake imefanya utafiti kwa mikoa mbalimbali kuangalia fursa zilizopo kama vile kilimo na utalii, na hivyo, imejipanga kuwawezesha wateja hao kukopa kiasi wanachohitaji ili kuendeleza na kukuza uwekezaji katika mkoa yao.
Hata hivyo, alisema vigezo na masharti ya ukopaji yatakazingatiwa kabla ya kutoa mkopo kwa mteja.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya CBA TanzaniaGift Shoko akizungumzia suala la riba na wateja hao, alisema, benki yao haina tofauti na benki zingine na kwamba wamechukua hatua ya kupunguza.
Alisema baadhi ya wateja wao tayari wameshapata barua za kuwajulisha kuhusu punguzo hilo.
Akizungumzia kuhusu madai ya kufungwa kwa matawi yao mikoani, Shoko alisema, walichofunga siyo matawi isipokuwa huduma zilizokuwa zikitolelwa na mawakala.
Alisema huduma za mawakala zilizokuwa zikitolewa Tunduma, Mtwara na Moshi ndizo zilifungwa, lakini hata hivyo, alisema wateja wao wanaendelea kupata huduma kupitia huduma za kibenki kwa njia ya mtandao.
Post A Comment: