Klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo Aprili 29, 2018 jijini Dar es salaam.
Goli la Simba limefungwa na Erasto Nyoni kunako dakika ya 37 kipindi cha Kwanza kwa makosa ya mabeki wa Yanga.
Hata hivyo mchezo huo ulionekana kuwa sawa kwa timu zote mbili kwani timu hizo zilionekana kushambuliana kwa zamu.
Kwa matokeo hayo Simba SC wameendelea kujiimarisha kileleni kwenye msimamo wa VPL kwa alama 62 wakifuatiwa na Azam alama 49 na huku Yanga wakisalia nafasi ya tatu kwa alama 48.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: