Kuafuatia kitendo cha mchezaji na beki wa Yanga, Kelvin Yondani, kumtemea mate Asante Kwasi katika mchezo wa ligi dhidi ya Simba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa tamko.

Kupitia Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amesema kuwa bado hawajapokea malalamiko kutoka Simba kuhusiana na suala hilo.

Mbali na ripoti kutoka Simba, Ndimbo ameeleza kuwa wao hutegemea pia ripoti ya Kamisaa wa mchezo husika ili kuja kuifanyia tathmini na kuja wapi kulikuwa na mapungufu ili yaweze kufanyiwa kazi.

Akizunguza jana jioni, Ndimbo amesema kuwa kama Simba watafikisha malalamiko yao, taratibu zingine za kihatua zitafuata ila kwa sasa hawawezi kufanya chochote.

Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumapili, Yondani alionekana kumtemea mate Kwasi ambaye hakuonesha kujibu mapigo ikiwa ni kipindi cha kwanza cha mchezo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: