Baada ya msanii Alikiba kuoa, maneno mengi na maswali yamekuwa yakielekezwa kwa mrembo Jokate Mwegelo.
Sababu
ni kwamba mara kadhaa mrembo huyo alidaiwa kuwa katika mahusiano na
Alikiba, hivyo kitendo cha Alikiba kuoa mwanamke mwingine kilizidi
kuibua mijadala ya hapa na pale kuhusu Jokate.
Sasa
muimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha amemuelezaJokate
kuwa asijali kwa kuwa ndoa inakuja, hata hivyo haijafahamika iwapo ni
yao wawili au laa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
“Usihofu Mungu hajakuacha Jokate Mwegelo yakwetu inakuja, tv zote zitakuwa live ukumbini hadi wasafi tv,” amesema Mbasha.
Katika
kuhadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa March 20, 2018 Jokate
aliweka wazi kuwa yupo mbioni kuolewa ingawa hakuweka wazi ni nani
atahusika katika ndoa hiyo.
Utakumbuka
pia muimbaji Mbasha kwa sasa hayupo katika ndoa na hii ni baada ya
kuachana na aliyekuwa baby mama wake, Madam Flora ambaye aliolewa April
30, 2017 na Daudi Kusekwa.
Post A Comment: