Na George Mganga

Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Azam Complex kwa wenyeji Azam FC kushindwa kutamba mbele ya Njombe Mji FC baada ya kulazimishwa suluhu ya 0-0.

Mchezo huo ulikuwa wa kasi kwa timu zote mbili kuonesha kupambana kutafuta matokeo lakini milango ilikuwa ni migumu kufungika.

Mnamo dakika ya 27 ya mchezo, Azam FC walipata penati ambayo ilipigwa na Nahodha Himid Mao lakini ilidakwa na kipa wa Njombe Mji.

Matokeo hayo yamezipa timu zote alama moja huku Azam ikifisha pointi 46 ikisalia katika nafasi ya 3 chini ya Yanga iliyo na 46.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: